top of page
Matundasi ASM Development Company Limited (MADC) ni kampuni inayojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa madini katika Mkoa wa Mbeya, wilaya ya Chunya.

FUNDI MAKENIKA WA MITAMBO MIKUBWA DARAJA LA III (Heavy Duty
Mechanic III) Nafasi Moja (01)

Chunya, Mbeya, Tanzania

Job Type

Fundi

Workspace

Chunya, Mbeya, Tanzania

Requirements

  1. Awe na cheti cha kuhitimu kidato cha nne (CSEE) au zaidi.   

  2. Awe amehitimu mafunzo ya ufundi stadi wa Daraja la III (Trade Test Grade III) au  NVA Level I au II katika fani ya Heavy Duty Mechanics au Mechanical Engineering  kutoka VETA au taasisi nyingine inayotambulika. 

  3. Uzoefu wa angalau mwaka mmoja  (01) katika kazi ya matengenezo ya mitambo  mikubwa kama vile Bulldozer, Excavator, Tractor, Grader na Malori Makubwa ya  Migodini (Mining Dump Trucks).   

  4. Uwezo wa kufanya kazi chini ya usimamizi wa mafundi waandamizi.   

  5. Uwezo wa kutambua matatizo madogo ya mitambo kama vile injini, breki, mfumo wa  maji (hydraulics), mfumo wa mafuta, n.k.   

  6. Uwezo wa kufanya ukaguzi wa kawaida (daily inspection) wa mitambo mikubwa.   

  7. Uwezo wa kutumia zana za kawaida za kazi kama vile spana, koleo, jack, na torque  wrench.  

  8. Uelewa wa kanuni za usalama kazini (HSE) katika mazingira ya karakana au mgodini.   

  9. Awe tayari kujifunza zaidi na kuboresha ujuzi wake kwa mafunzo ya daraja la juu  (Daraja II na I).   

  10. Leseni ya udereva daraja C au E kutoka katika chuo kinachotambulika.    

  11. Awe na umri usiozodi miaka 30.

About the Company

Matundasi ASM Development Company Limited (MADC) ni kampuni inayojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa madini katika Mkoa wa Mbeya, wilaya ya Chunya.
bottom of page